Monday, January 15, 2018

Upishi wa tambi

Tambi za mayai ni moja kati ya chakula kizuri sana na huchukua muda mfupi sana katika uandaaji wake. 

MAHITAJI
  • Tambi nusu paketi
  • Vitunguu maji 2 vikubwa 
  • Keroti 1
  • Hoho 1
  • Vitunguu swaumu
  • Njegere zilizochemshwa nusu kikombe
  • Mafuta kwa kiasi upendacho
  • Mayai 2
  • Chumvi kwa ladha upendayo 

NJIA
1.Chemsha maji ya moto sana, ongeza chumvi na mafuta kidogo, weka tambi kwenye maji hayo chemsha hadi ziive. chuja maji yote ili kupata tambi kavu.

2. Piga mayai katika bakuli kisha weka pembeni.

3. Katika kikaango, weka mafuta, vitunguu maji, vitunguu swaumu, hoho, na keroti, kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mchanganyiko huo hautakiwi kuiva sana.

4. Ongeza tambi na njegere katika kikaango, geuza kila mara ili kuchanganya.

5. Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika hadi mayai yaive na tambi ziwe kavu. Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani ili mayai yapate kuiva na kushikana na tambi vizuri .Tayari kwa kulaaaaaaa.



No comments:

Post a Comment

Upishi wa tambi

Tambi za mayai ni moja kati ya chakula kizuri sana na huchukua muda mfupi sana katika uandaaji wake.  MAHITAJI Tambi nusu paketi Vitung...